Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585763

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fainali Super Cup, ni Madrid na Athletic Bilbao

Fainali Super Cup, ni Madrid na Athletic Bilbao Fainali Super Cup, ni Madrid na Athletic Bilbao

Athletic Bilbao itapepetana vikali na Real Madrid katika mchezo wa fainali ya Kombe la Hispania Super Cup mchezo utakaopigwa Jumapili Januari 16.

Bilbao wamepata nafasi hiyo baada ya kuifunga goli 2-1 klabu ya Atletico Madrid kwenye mechi iliyopigwa Alhamis ambapo sasa Mabingwa hao watetezi wa Kombe hilo Wana fursa ya kuondoka na taji msimu huu kwenye Uefa na La Liga.

Bao la kwanza lilikuwa la Atletico Madrid kupitia kwa kiungo mshambuliaji tena ghali Joao Felix, kabla ya dakika za 77 Yeray Alvarez kusawazisha na Nico Williams kufunga goli la ushindi dakika tisa kabla ya kabumbu kumalizika.

Real walipata tiketi hiyo baada ya kuifunga Barcelona goli 3-2 kwenye muda wa ziada.