Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572872

Michezo Mingine of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fallon Sherrock atinga nane bora Grand Slams Darts

Fallon Sherrock (kulia) Fallon Sherrock (kulia)

Mcheza Darts wa Uingereza, Mwanamama Fallon Sherrock ameweka historia katika michuano ya Dunia ya Darts inayoendelea baada ya kupata ushindi dhidi ya Mensu Suljovic pale Wolverhampton.

Fallon Sherrock, 27 ameandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuingia robo fainali ya Grand Slam ya Darts baada ya kutoka nyuma kwa 2-0 na kushinda 10-5.

Hii ni mara ya pili ndani ya wiki moja kushinda mechi kwa mizunguko mitano zaidi baada ya kufanya hivyo pia katika ushindi wke siku ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mike de Decker.

“Sijui nafanyaje hivi, Najivunia mwenyewe,” alisema Sherrrock

“Haikuwa mechi kubwa sana lakini nachukua ushindi.

“Nilikuwa nyuma kwa 2-0 dhidi yake katika Mashindano ya Dunia na nikarejea, Nilihitaji kutulia na kucheza.” Aliongeza

Sherrock atachuana na Bingwa wa dunia wa 2020, Peter Wright siku ya Jumapili.