Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 09Article 541843

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Fomu ugombea Urais ZFF sasa hadi Juni 12

Kuongeza kwa  muda wa zoezi hilo ni ili kuwapa fursa wadau wa soka kujitokeza zaidi kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo.

Mpaka sasa waliochukua fomu  za kuwania nafasi hiyo ni wagombea watatu ambao ni Abdulatif Ali Yasin ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mjini Magharibi, Suleiman Shabaan Suleiman, Mwenyekiti wa timu ya Chuoni FC na Suleiman Mahmoud Jabir, kocha na mkufunzi wa michezo Zanzibar.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya ZFF, Makungu Omar Makungu, alisema kiwango cha elimu kilichowekwa kwa wagombea urais ni shahada, ambacho ni kwa mujibu wa Katiba ya ZFF na kwamba hali ya mpira wa sasa duniani kote unaendeshwa kwa kutegemea zaidi elimu tofauti na uzoefu.

Join our Newsletter