Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 13Article 557221

Habari za michezo of Monday, 13 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

GSM, Hersi watua msibani Karimjee

GSM, Hersi watua msibani Karimjee GSM, Hersi watua msibani Karimjee

Mdhamini wa klabu ya Yanga, Ghalib Said 'GSM' ameibuka katika msiba wa Zacharia Hanspope saa 7:10 mchana huu wakati waombolezaji wakiendelea kutoa Salamu za rambirambi.

GSM amewasili viwanja vya Karimjee akiambatana na Mhandisi Hersi Said na kuketi katika viti wakati Mjumbe wa bodi ya Simba Cresentius Magori akimzungumzia marehemu.

Magori amesema msiba wa Hans Poppe ni mkubwa na kamwe wa kuuziba hakuna "Hans Poppe kafanya makubwa Sana ndani ya Simba tutamkumbuka kwa mengi na mazuri aliyoyafanya," amesema.