Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554425

Soccer News of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"GSM wamewekeza kwenye Uchumi" - Ally Mayai

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Mchambuzi, Ally Mayai Mchezaji wa zamani wa Yanga na Mchambuzi, Ally Mayai

Nyota wa zamani wa Timu ya Taifa na Klabu ya Yanga Ally Mayai Tembele amesema GSM wamewekeza zaidi kwenye uchumi wa Klabu ya Yanga hivyo ni rahisi kuona mabadiliko katika klabu hiyo.

Ally ameyasema hayo kutokana na usajili mkubwa wa wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ambao wamesajiliwa na Yanga msimu huu na kutambulishwa katika kilele cha "Siku ya Mwananchi".

"Yanga ina uchumi imara kwa sasa na hii ni kutokana na uwekezaji mzuri ambao umefanywa na GSM, kwa sababu uwekezaji wenye faida ni ule unaohusisha maeneo ya msingi kama usajili wa kocha mzuri, Wachezaji ,Vifaa vya mazoezi na kambi vile vile na ndivyo ambavyo GSM wamefanya" amesema Ally

Kauli hiyo ya Ally Mayai imekuja kutokana na wadau mbali mbali wa Soka nchini kuhoji Udhamini wa GSM ndani ya Klabu ya Yanga kama kweli una tija ama la.