Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 20Article 558646

Soccer News of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Geita Gold wampa ulaji Kivuyo

Afisa Habari wa Geita Gold, Hemedy Kivuyo Afisa Habari wa Geita Gold, Hemedy Kivuyo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Mhe. Zahara Michuzi amemtambulisha Mwanahabari mbobezi na mwandamizi katika maswala ya soka, Hemedy Kivuyo kuwa Msemaji Mkuu wa timu hiyo wakati Kikosi chao kikijiandaa na Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la ASFC msimu wa 2021-2022.

Kivuyo ametambulishwa katika Tamasha la Geita Gold Day 2021 sambamba na kutambulishwa Wachezaji wapya watakaotumikia timu hiyo kwenye msimu huu wa mashindano.

Akizungumza kwenye tamasha hilo, Mhe. Zahara amesema ni rasmi Kivuyo atakuwa Msemaji wa Mabingwa na matajiri wa dhahabu (GGFC) wakati tukijiandaa kucheza Ligi Kuu na Mashindano mengine hapa nchini.

“Karibu sana kwenye familia ya Mabingwa Mr. Hemedy Kivuyo, Wanageita wana imani kubwa na wewe na wasubiri makubwa toka kwako”, ameeleza.

Kikosi cha Geita Gold FC kinachonolewa na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije kimepanda Ligi Kuu msimu huu wa mashindano wa 2021-2022 kwa mara ya kwanza wakitokea Ligi daraja la kwanza ambayo kwa sasa itatambulika kama Championship.

Hemedy kivuyo ni mwandishi wa Habari za Michezo aliewahi kufanya kazi na Vituo vya ITV na Redio One, vya Jijini Dar es Salaam, na anakumbukwa na wengi kutokana na mbwembwe zake katika utangazaji.

Bila shaka tutarajie kuona mpambano wa nje ya uwanja baina ya wasemaji wa vilabu msimu utakapoanza kama Masau Bwire, Haji Manara, Thobias Kifaru na Hemedy Kivuyo.