Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586051

African Cup of Nations of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ghana Waduwazwa na Gabon Afcon 2021

Mchezo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 Mchezo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1

Gabon wamefanikiwa kuambulia alama nne katika mechi mbili za kwanza hatua ya makundi Kundi C baada ya mchezo wa Ijumaa dhidi ya Ghana kumalizika kwa sare ya goli 1-1 mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 ambayo yanaendelea Cameroon.

Licha ya kumkosa mshambuliaji na nahodha Pierre-Emerick Aubameyang Gabon wameendelea kuonyesha kiwango kizuri na sasa pengine wanahitaji alama moja pekee katika mechi moja kufuzu hatua ya 16 bora.

Kwa upande wa Ghana wanavuna pointi moja pekee kwenye mechi mbili ukiwa ni wakati mgumu kwao, walifungwa 1-0 na Morocco kabla ya kulazimishwa sare na Gabon.

Magoli kwenye mechi hiyo yalitanguliwa na bao la Ghana kutoka kwa mshambuliaji Andrew Ayew kunako dakika ya 18 akipokea pasi kutoka kwa Thomas Partey bao la kusawazisha likitupiwa na Jim Allevinah dakika ya 88.

Kwa matokeo hayo, Morocco wanaongoza kundi C wakiwa na alama 6 baada ya ushindi kwenye mechi mbili, Gabon alama 4, Ghana alama 1 na Comoros pointi sifuri.

Mechi za mwisho, itakuwa Januari 18 ambapo Ghana watacheza na Comoros na Morocco watahitimisha na Gabon.