Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572536

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Giovanni van Bronckhorst kumrithi gerrard Rangers

Giovanni van Bronckhorst Giovanni van Bronckhorst

Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Giovanni van Bronckhorst anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Rangers baada ya kufikia makubaliano ya uongozi wa klabu hiyo.

Giovanni van Bronckhorst ambaye pia amewahi kukitumikia kikosi cha Rangers (1998-2001) anarudi tena Ibrox kuchukua mikoba ilioachwa na Steven Gerrard aliyejiunga na klabu ya Aston Villa.

Van Bronckhorst alionekana London siku ya jumamosi ambapo inasemekana alifanya mazungumzo chanya na uongozi wa Klabu ya Rangers kabla ya kurejea Uholanzi.

Van Bronckhorst alijiunga na Arsenal na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu, kabla ya baadae kujiunga na Barcelona na hatimae Feyenoord.

Rangers wanaongoza kwa alama 4 mbele ya Celtic katika msimamo wa ligi ya Scotland baada ya michezo 13. Mechi inayofuata itakua dhidi ya Hibernian kwenye nusu fainali ya kombe la ligi pale Hampden Park.