Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572596

Soccer News of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Godin kurudi tena Hispania

Diego Godin Diego Godin

Mchezaji wa Kimataifa wa Uruguay Diego Godin, amezungumza na mchezaji mwenzie wa timu ya Cagliari kuwa ana mpango wa kurudi tena Hispania.

Beki huyo wa kati ambaye aliwasili Cagliari akitokea kwenye timu ya Inter Milan mwezi septemba 2020 lakini amekuwa na presha kubwa kwa muda wote kwa sababu ya timu anayochezea kuwa kwenye nafasi za kushuka daraja.

Godin mwenye miaka 35 ameshindwa kuisaidia timu yake ya sasa kuweza kupanda kwenye msimamo waligi kuu ya Serie A baada ya kuwa kwenye nafasi za chini hata baada ya kucheza michezo 12 mpaka sasa.

Godin ameichezea timu ya taifa ya Uruguay michezo 153, na aliwasiri nchini Italia julai 2019 baada ya kusajiliwa na timu ya Inter Milan iakiwa mchezaji huru. Kwa sasa kuna tetesi kuwa kuna klabu kwenye ligi ya La Liga imeonesha nia ya kutaka kumsajili.