Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 28Article 540391

Habari za michezo ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Gomes: Tutamfunga yeyote

Gomes: Tutamfunga yeyote Gomes: Tutamfunga yeyote

BAADA ya kikosi cha Simba kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes ametamba kuwa safari ya kutetea ubingwa wao imeanza na hawana hofu na timu yoyote.

Simba ndio bingwa mtetezi wa taji hilo na itacheza na Azam FC katika nusu fainali ya michuano

hiyo baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa robo fainali uliopigwa uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Gomes raia wa Ufaransa alisema kiwango kinachooneshwa na wachezaji wake kinampa imani ya kutetea ubingwa huo bila kujali wapinzani ambao atakutana nao katika hatua mbili zilizobaki.

“Natambua tunakwenda kucheza na Azam FC, natambua uwezo walionao, lakini wapinzani watambue Simba hii ni tofauti na waliyoizoea inaweza kucheza na timu yoyote na kushinda tena kwa idadi kubwa ya mabao,” alisema Gomes.

Kocha huyo alisema kiwango walichokionesha kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ilikuwa ni sehemu ya ubora walionao hivi

sasa kutokana na ushiriki wao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali na Kaizer Cheifs ya Afrika Kusini wiki iliyopita.

Gomes alisema pamoja na ubora walionao Azam, lakini haoni kama kuna kikwazo cha wao kushindwa kufikia malengo yao msimu huu ambayo ni kutetea taji hilo na kubeba ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aidha, kocha huyo amemwagia sifa kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison kutokana na kiwango bora alichoonesha kwenye michezo miwili iliyopita dhidi ya Kaizer Chiefs na Dodoma Jiji FC.

Alisema mchezaji huyo ana mchango mkubwa kwenye kikosi chake na ana amini ataisaidia timu hiyo katika mechi zilizobakia kabla ya msimu kumalizika.

Join our Newsletter