Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554356

Soccer News of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gomes amuonya Mkude

Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude akijifua Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude akijifua

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes ametoa somo kwa kiungo mkabaji wa timu hiyo, Jonas Mkude kutokana na mwennendo wa mfululizo wa makosa ya kinidhamu ndani ya kikosi hicho na atakua akifatilia kwa karibu mwenendo wa Mchezaji huyo.

Mkude ambaye mwishoni mwa msimu uliopita, aliingia katika mzozo na benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na wachezaji wenzake kutokana na kufululiza kwa matukio yake ya utovu wa nidhamu kiasi cha uongozi wa timu hiyo kumsimamisha kwa muda hadi kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Simba chini ya Kamanda mstaafu wa Dar es Salaam, Seleman Kova.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Gomes ameamua kumuweka chini kiungo huyo na kumpa masharti yake ikiwa atahitaji kuendelea kucheza Simba.

Taarifa za kina zinaeleza kuwa Gomes alitoa masharti hayo kwa kuwa hataki kuwagawa wachezaji wake kupitia matatizo ya utovu wa nidhamu kwani mipango yake ni kishughulikia kwenye levo moja.

“Ni kweli mwalimu Gomes, alikaa kikao na Mkude hii ni kutokana na masuala yake la utovu wa nidhamu, amempa masharti kwa kuwa mwalimu hataki kuona anaigawa timu upande wa wachezaji ambao mwenyewe anataka wawe kwenye daraja moja ili kuweza kupambania timu".

“Mwalimu amemuambia hataki kusikia jambo lolote la utovu wa nidhamu kutoka kwake kama alivyofanya msimu uliopita, amemwambia anataka kumuona wa kwanza katika kila jambo ambalo timu hiyo itakuwa inafanya kwa wakati huo,” amesema mtoa taarifa.

Klabu ya Simba kwa sasa ipo nchini baada ya kurejea kutoka nchini Morocco ambako waliweka kambi kujiandaa na msimu ujao, na kwa mujibu wa Kaimu Afisa Habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema Timu hiyo itaweka kambi kwa mara nyingine hapa hpa nchini wakijiandaa na msimu mpya.