Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558271

Soccer News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gomes ashamalizana na Yanga, tusubiri siku tu

Chriss Mugalu Chriss Mugalu

Unaambiwa huko mazoezini kwa Simba, Kocha Mkuu, Didier Gomes, kila kukicha alikuwa akiwapa mbinu mpya wachezaji wake, Chris Mugalu, Duncan Nyoni na Pape Ousmane Sakho kwa ajili ya kuwaua Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Septemba 25, mwaka huu, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba iliyoweka kambi Arusha, ikiwa huko imecheza michezo mitatu ya kirafiki ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2021/22, Simba imefanikiwa kushinda michezo miwili dhidi ya Fountain Gate (1-0) na Aigle Noir ya Burundi (2-1), huku ikishindwa kufungana na Coastal Union.

Taarifa kutoka ndani ya kambi ya Simba, zinasema kwamba, Gomes amefanikiwa kutengeneza safu mbili tofauti za mauaji kuelekea mchezo dhidi ya Yanga, ambapo tayari amemuingiza kikosini kiungo, Duncan Nyoni ili acheze karibu na Chris Mugalu.

“Kocha amelazimika kumuondoa pembeni Nyoni na kumsogeza karibu na Mugalu, ikiwa ni mbinu sahihi kabisa ya maandalizi yake kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

“Pamoja na Gomes kuwaanda viungo Rally Bwalya na Sadio Kanouté, pia kuna pacha nyingine ya Mugalu, Nyoni na Sakho, ambayo itakuwa maalumu kabisa kwa ajili ya kufanya mauaji mbele ya Yanga,” kimesema chanzo.