Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 26Article 544390

Habari za michezo of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Gomes awapangia Azam kikosi cha mauaji

Gomes awapangia Azam kikosi cha mauaji Gomes awapangia Azam kikosi cha mauaji

KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes tayari amepanga kikosi cha wachezaji 11 watakao ingia uwanjani dakika chache zijazo kucheza nusu fainali ya kombe la Azam (ASFC) dhidi ya Azam Fc.

Katika mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Majimaji Songea, Gomes amepanga wachezaji ambao mara nyingi wamekuwa wakianza kwenye kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi.

Langoni amemuanzisha kipa Aishi Manula, na kuwapanga Mohammed Hussein, Tshablala na Shomari Kapombe kucheza kama mabeki wa pembeni.

Eneo la mabeki wa kati, Gomes amewaanzisha Joash Onyango na Paschal Wawa huku Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin wakichezeshwa kama viungo wa kati chini.

Rally Bwalya, Cloatus Chama na Luis Miquissone wamepangwa kucheza eneo la mbele ya viungo wakabaji wawili wakati John Bocco akisimama kama mshambuliaji pekee kwenye mfumo wa 4-2-3-1.

Mtanange huo unatarajiwa kuanza saa 9:30 jioni katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ambao hadi sasa umefurika mashabiki.