Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 16Article 557947

Soccer News of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Guardiola achukizwa na mashabiki City

Guardiola achukizwa na mashabiki City Guardiola achukizwa na mashabiki City

MANCHESTER, ENGLAND. Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amekuwa mbogo akiwaomba mashabiki kuacha uvivu wa kutokwenda uwanjani kuangalia mechi za timu yao.

Guardiola ameonekana na kutofurahishwa na matokeo ya mabao 6-3 waliyopata hapo jana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig, baada ya timu yake kuruhusu mabao matatu huku akidai chanzo ni mashabiki hawakujitokeza kwa wingi.

Takwimu zilionyesha mashabiki 38,062 tu waliingia uwanjani kuangalia mchezo huo ulichezwa uwanjani Etihad.

“Tunahitaji mashabiki wengi uwanjani, hii itasaidia wachezaji kucheza kwa bidii, hata kama wachezaji watachoka nguvu ya mashabiki itawainua na kuwapa moyo,” alisema Guardiola.