Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 12Article 585259

Soccer News of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Guinea Bissau, Sudan hakuna mbabe AFCON

Sudan vs Guinea Bissau zatoka sare ya bila kufungana Sudan vs Guinea Bissau zatoka sare ya bila kufungana

Guinea-Bissau katika dakika za mwisho wamepoteza nafasi ya kuondoka na alama tatu kufuatia kukosa tuta dhidi ya Sudan katika dakika ya 82 ya mchezo kwenye mechi ya kwanza Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2021 mtanange wa Kundi C.

Kiungo “staa” Pele alikosa tuta hilo baada ya kuokolewa na mlinda mlango wa Sudan Ali Abou Achrine, huku Piqueti akikosa hata mpira uliorudi baada ya kupanguliwa na kipa.

Tuta la mchezo huo liliamuliwa na mwamuzi kwa kile kilichoonekana Abou Achrine kumfanyia madhambi Steve Ambri kwenye eneo la hatari.

Matokeo hayo yanaifanya Sudan ambayo inashiriki Afcon kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, Guinea Bissau kuwa sawa alama baada ya sare hiyo tasa wakati Nigeria wakiwa kileleni, Misri inaburuza mkia katika Kundi C.

Mechi zijazo, itakuwa baina ya Nigeria na Sudan wakati ambao Misri watakuwa na Guinea Bissau.