Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584797

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Guinea sahani moja na Senegal AFCON

Wachezaji wa Guinea wakipongezana Wachezaji wa Guinea wakipongezana

Guinea imeanza mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2022 kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kwanza wa Kundi B uliopigwa jana Jumatatu Januari 10.

Bao pekee kwenye mechi hiyo limefungwa kunako dakika ya 35 na Issiaga Sylla baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jose Kante kwenye mtanange uliopigwa dimba la Bafoussam.

Guinea, inayoongozwa na kiungo mshambuliaji wa Liverpool Naby Keita, inaungana na Senegal kileleni mwa msimamo wa Kundi B baada ya Senegal kushinda bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe zote zikiwa na alama tatu.