Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 28Article 560227

Soccer News of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gwiji wa zamani Liverpool, afariki akiwa na miaka 83

Gwiji wa zamani wa Liverpool, Sir. Roger Hunt Gwiji wa zamani wa Liverpool, Sir. Roger Hunt

Klabu ya Liverpool inaomboleza msiba wa Gwiji wake wa zamani Roger Hunt. Hunt alichezea Liverpool miaka takribani 50 iliyopita, lakini rekodi yake ya kupachika mabao kwenye Ligi Kuu ya England kwa mchezaji wa Liverpool bado haijavunjwa.

Mwaka 1966 alikuwa sehemu ya kikosi cha England kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Wiki mbili baadaye akajiunga na kikosi cha Liverpool kujiandaa na msimu mpya.

Roger Hunt anashika nafasi ya pili kwa wafungaji bora wa muda wote wa Liverpool akiwa amefunga magoli 285 akicheza michezo 492.

Roger Hunt aliezaliwa mwaka 1938 amefariki akiwa na umri wa miaka 83. Amewahi kufundishwa pia na Kocha Bill Shankly.