Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585943

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Haji Mwinyi: Niko Tayari Kusaini Yanga

Haji Mwinyi Haji Mwinyi

HAJI Mwinyi beki wa kazi chafu ndani ya kikosi cha KMKM ya Zanzibar ameweka wazi kwamba yupo tayari kusaini Yanga kwa kuwa kazi yake ni soka.

Ikumbukwe kwamba nyota huyo aliwahi kucheza ndani ya Yanga kabla ya kuachwa kwa sasa maisha yake yanaendelea ndani ya kikosi cha KMKM.

Beki huyo amesema: “Kwa sasa nipo na timu yangu hii nikiendelea kutimiza majukumu yangu, lakini ikitokea Yanga wakahitaji saini yangu nipo tayari kujiunga nao kwani mpira ni kazi yangu.

“Kuondoka mahali haina maana kwamba huwezi kurudi, jambo lolote linawezekana na huku nilipo sisi tunapambana na ukitazama kwenye ligi bado hatujafungwa wala hatukamii mechi bali ni mipango.”

Walipokutana na Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi KMKM walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2, ambapo Haji aliwapa tabu washambuliaji wa Yanga ikiwa ni pamoja na Heritier Makambo pamoja na kiungo mpya Dennis Nkane.