Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553684

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Haji ukituvuruga nasi tunakuvuruga" -DC Jokate

DC wa Temeke, Jokate Mwegelo DC wa Temeke, Jokate Mwegelo

Leo katika uzinduzi wa jezi mpya za klabu ya Yanga alifika Shabiki wa kutupwa wa Klabu hiyo ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo.

Jokate alipewa nafasi ya kuzungumza machache katika hafla hiyo na aliposalimia alimpa taarifa msemaji mpya wa Klabu hiyo ambae ametokea Klabu ya simba, Haji Manara.

"Yanga oyee, Haji umekuja kuleta vurugu Yanga eeh, sasa nikwambie ukituvuruga na sisi tutakuvuruga, nikiwa kama mwana TMK, maeneo ambayo mnafanya shughuli nyingi za kimpira nimeweza kufarijika kuwepo mchana wa leo hapa, nawapenda sana niwatakie siku njema". amesema Jokate

Uzinduzi huo umefanyikia katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Leo Agosti 25 na Msemaji mpya wa Klabu hiyo Haji Manara ndio aliekua mshareheshaji.