Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 16Article 551743

Soccer News of Monday, 16 August 2021

Chanzo: salehejembe.blogspot.com

Hali ya hewa Morocco kwa Simba Fresh tu

Mchezaji wa Simba akiwa mazoezini Mchezaji wa Simba akiwa mazoezini

KIKOSI cha Simba kinaendelea na mazoezi nchini Morocco kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22 huku kocha akibainisha kuwa hali ya hewa haina tatizo kwao ni fresh tu.

Didier Gomes anna kazi ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na kuvunja rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu wa 2020/21, Simba ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa jambo ambalo limeifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa zile 10 ambazo hazitaanzia hatua ya awali.

Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambaye ni Al Ahly kutoka Misri alitwaa ubingwa huo mbele ya Kaizer Chiefs ambayo iliitoa Simba hatua ya robo fainali na zote zilikuwa kundi moja katika hatua ya makundi.

Gomes amesema kuwa hali ya hewa pamoja na kambi kwao ni nzuri jambo linalowapa nafasi ya kufanya vizuri msimu mpya.