Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 26Article 553927

Soccer News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hapatoshi Fainali ndondo Cup

Mchezo wa fainali Ndondo Cup, kuchezwa wikiendi hii Mchezo wa fainali Ndondo Cup, kuchezwa wikiendi hii

Yale Mashindano ya kuibua vipaji kwa Timu zinazopatikana katika jiji la Dar es Salaam na yasiyoisha vituko na vioja maarufu kama Ndondo Cup, sasa yamefikia hatua ya Fainali.

Wababe waliofanikiwa kupenya katika hatua hiyo ni Tabata All Stars kutoka Ilala na ikiongozwa na Nahodha wake nguli wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba dhidi Vifundo FC kutoka Wilaya ya Temeke.

Katika Fainali hiyo itakayopigwa siku ya Jumamosi Agosti 28, katika Uwanja wa bandari, Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 20.

Viingilio katika mchezo huo unaohisiwa kuteka hisia za Wana-Dar es salaam ni shilingi 3000.