Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585691

Habari za michezo of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Harmonize: Sijamtuma Mtu

Harmonize: Sijamtuma Mtu Harmonize: Sijamtuma Mtu

C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Music, Harmonize au Konde Boy Mjeshi amefunguka kwamba hawezi kumtuma mtu akamzungumzie mtu f’lani kwa sababu haimsaidii chochote.

Harmonize ameyasema hayo baada ya kuulizwa kama huwa anawatuma machawa kuwazungumzia mahasimu vibaya wake?

Katika majibu yake, Harmonize anasema; “Ukiona mtu yeyote anaenda kumzungumzia mtu fulani basi ujue ni maamuzi yake na mimi binafsi siwezi kumtuma mtu yeyote akamzungumzie mtu f’lani kwa sababu hainisaidii.

“Ukiona mtu anatuma watu wamzungumzie mtu f’lani, basi ujue anawaza ndani ya boksi,” anasema Konde Boy.