Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 16Article 557977

Mpira wa Kikapu of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hasheem Thabeet atajwa kikosi cha "Dream Team" Taifa Cup

Hasheem Thabeet atajwa kikosi cha Hasheem Thabeet atajwa kikosi cha "Dream Team" Taifa Cup

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Hasheem Thabeet ametajwa kwenye kikosi cha mkoa wa Dar es Salaam 'Dream team' kitakachoshiriki mashindano ya taifa (Taifa Cup).

Katika kikosi hicho, Thabeet ambaye yuko nchini na amecheza Ligi ya mkoa (RBA) ametajwa kama mchezaji wa Savio akiwa miongoni mwa nyota 30 wa timu hiyo walioitwa kuundwa kikosi cha Dream team.

Timu hiyo ambayo itanolewa na kocha mkuu, Christiant  Yakobo akisaidiana na Mohammed  Yusuph na Mohammed  Mbwana ina wachezaji wanne wa nafasi ya center anayocheza Hasheem, wengine ni Jimmy Brown wa Kurasini Heat, Haji Mbegu wa Ukonga Kings na Daudi Machanya wa Outsiders.

Kwenye nafasi ya point guard waliochaguliwa ni Alinani Andrew wa ABC, Evance Davis wa Oilers, Charles Paul wa Savio, Ali Faraji wa Vijana, Omary Sadiki wa JKT, Deo Alfred wa Kurasini Heat na Nicas Buhatwa wa Outsiders.

Upande wa Shooting Guard ni Eric Lugola wa Ukonga Kings, Isaya Wiliam wa Mchenga, Ronardo Kidobwe wa Viaja, Oscar Anthony wa Savio Colnelus Peter wa DTB, pRUDENSIUS sHIJA WA jkt, Philbert Mwaipungu wa ABC na Trophy Chemundu wa Pazi.

Wanaocheza nafasi ya Small forward ni Enrico Augostino wa ABC, Jacob Linus wa JKT, Denis Chibura wa Pazi, Amini Mtambo wa Savio na Mussa Chacha wa JKT.

Nafasi ya power forward ni Omary Juma na Mosses Jackson wa ABC, Fadhiri Chuma wa Kurasini Heat na Jackson Brown wa JKT.

Chama cha mpira wa kikapu Dar es Salaam (BD) pia kimechagua kikosi cha nyota 26 wa timu ya wanawake ambayo itaongozwa na kocha Ashrafu Haroun akisaidiwa na Lucy Agostino na Elizabeth Mwasenyi kwenye mashindano ya taifa mjini Dodoma.

DB Liones katika kikosi hicho imetoa nyota saba ambao ni Rehema Silomba, Naima Omary, Hope Mericka, Maria Kihivo, Diana Mwendi, Jasmine Bablia

Wakati kutoka Vijana Queens (VBQ) ni Noela Renatus, Maria Komba,  Khadija Karambo, Tumain Ndosi, Diana Katembo, Neema Yacobo na Angel Minja

JKT Stars walioitwa ni Winfrida Chikawe, Frida Zabron, Faraja Malaki, Jesca Julius, Pendo Mpera, Celina Nollo, Irene Kapambala, Sarah Budodi, Joyce Kaila na Peninah Mayunga. Na Ukonga Queens ni Maria Kihivyo, Monalisa Kaijage, Lilian Mwaluswaswa, Amina Kaswa na Witness Edward

Katibu Mkuu wa BD, Mpoki Mwakipake amesema timu hiyo itaanza maandalizi wakati wowote kanzia sasa kujiandaa na mashindano ya Taifa ambayo msimu huu wamedhamiria kurejesha makali ya Dream team ambayo Ligi yake kwa sasa iko hatua ya nusu fainali kwa timu za ABC na Ukonga Kings na Savio na JKT kuchuana kusaka bingwa.