Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 20Article 558637

Soccer News of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Hatima ya Balama Yanga mikononi mwa kocha Nabi

Balama Mapinduzi. Balama Mapinduzi.

IMETHIBITISHWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi tayari amekamilisha programu maalum za mazoezi binafsi ambazo alipewa na benchi la ufundi na kujiunga na wenzake, hivyo hatima yake ndani ya kikosi cha Yanga ipo chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi.

Balama alipata jeraha la enka katika mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda mwezi Juni mwaka jana, na kufanyiwa upasuaji mara mbili hivyo kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya mwaka sasa.

Daktari wa klabu ya Yanga, Shecky Mngazija alisema: “Kwa sasa Balama Mapinduzi tayari amemaliza programu binafsi za mazoezi maalum aliyokuwa amepewa na benchi la ufundi na ameanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake.

“Hivyo kutokuonekana kwake hakuna mahusiano na majeraha bali ni maamuzi ya kocha mkuu ambaye kutokana na utayari wa mchezaji husika anaweza kumpa nafasi.”