Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584953

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Henderson achoka kusugua benchi United

De Gea (kushoto) akiwa na Dean Henderson (kulia) De Gea (kushoto) akiwa na Dean Henderson (kulia)

Hii ndio nguvu ya madaraka. Kocha wa Manchester United, Ralf Rangnick, amelikataa ombi la Dean Henderson kuondoka United mwezi huu.

Henderson amejikuta akisugua benchi wakati huu ambao David de Gea anaendelea kuwa kwenye kiwango thabiti na muhimili muhimu kwa United. Akiwa na umri wa miaka 24 tu, Henderson amegonga milango ya Rangnick akiomba kuruhusiwa kuondoka klabuni hapo mwezi huu.

Ni kama amekuwa na nyota mbaya. Wakati anacheza Sheffield United kwa mkopo, De Gea alikuwa kwenye kiwango kibovu sana United. Baadae, Henderson alirejea United akiwa na imani ya kupewa mikoba ya kuwa kipa namba 1 Old Trafford. Kwa kunogesha hilo, Ole Gunnar Solskjaer alimpatia mkataba mpya kipa huyu. Lakini, mambo yamekuwa tofauti.

Rangnick amethibitisha kupokea ombi la Dean Henderson lakini, ameongeza kwa kusema kuwa – lengo lake ni kuendelea kumbakiza Henderson kwenye kikosi cha United walau mpaka mwishoni mwa msimu huu ndio kama klabu, watafanya maamuzi kwa kumshirikisha mchezaji husika.

Dean Henderson na Anthony Martial ni wachezaji wawili walioripotiwa kuweka wazi malengo yao ya kutaka kuondoka United mwezi huu.