Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584602

African Cup of Nations of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Hiki ndio kiasi cha pesa atakazolipwa mshindi wa AFCON

Hiki ndio kiasi cha pesa atakazolipwa mshindi wa AFCON Hiki ndio kiasi cha pesa atakazolipwa mshindi wa AFCON

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 imeanza huku idadi kubwa ya watangazaji wakijiandaa kuangazia tukio kubwa la kimichezo barani Afrika na shindano la tatu kwa ukubwa duniani la soka baada ya Kombe la Dunia la FIFA na Ubingwa wa UEFA, kutokea Cameroon hadi kuwafikia mamilioni ya mashabiki nchi 157.

Ingawa pesa za zawadi kwa ujumla hutazamwa kuvigusa vilabu pekee ulimwenguni, jumla ya Tsh. Bilioni 4.2 zimeongezwa kwenye zawadi kutoka hatua ya robo fainali hadi fainali za mwaka huu.

Sio hivyo tu, lakini zawadi mpya kwa washindi wa shindano hilo ni Tsh. Bilioni 11.5 - ikiwa ni ongezeko la dola 500,000 kutoka kwenye zawadi ya awali katika. Zaidi ya hayo, kadiri taifa linavyosonga mbele katika michuano hiyo, ndivyo wanavyopata fedha nyingi zaidi moja kwa moja, hivyo ni kwa manufaa yao kusonga mbele katika raundi hiyo sio tu kwa mafanikio uwanjani bali pia kwa ajili ya kuimarika kifedha.

Timu zitapokea kiasi gani kwa robo fainali?

Kila moja kati ya timu nane zitakazofuzu kwa robo fainali ya michuano hiyo itapata Tsh. Bilioni 2.7 (ongezeko la dola 175,000 kutoka kwenye zawadi ya awali katika toleo la 2019).

Timu zitapokea kiasi gani kwa nusu fainali?

Kila moja kati ya timu nne zitakazofuzu kwa nusu fainali ya michuano hiyo itapata Tsh. Bilioni 5.0 (ongezeko la Dola 200,000).”

Je! ni pesa gani ya zawadi ya kushinda AFCON 2021?

Mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 watapata zawadi ya Tsh. Bilioni 11.5, huku washindi wa pili watapata zawadi ya Tsh. Bilioni 5.7.

Pesa hizo zinatoka wapi?

Wafadhili ni muhimu, na kwenye michuano ya 33 la AFCON, TotalEnergies ndio wadhamini wakuu wa taji la mashindano hayo kama sehemu ya makubaliano yake ya ushirikiano wa miaka minane na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Ingawa CAF haijaweka wazi makusanyo ya wafadhili kwaajili ya udhamini wa watu binafsi, matarajio ni kwamba mapato yatakayopatikana kutoka kwa chapa zinazotaka kuhusishwa na wachezaji wakuu wa Afrika yataingiza zaidi ya dola za Kimarekani milioni 35 katika mapato kwa shirikisho la soka barani Afrika.