Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 17Article 552034

Soccer News of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hizo jezi za mazoezi tu jamani - Injinia Hersi

Kikosi cha Yanga kikiwa mazoezini nchini Morocco Kikosi cha Yanga kikiwa mazoezini nchini Morocco

Yanga imetumia jezi mpya ambazo hazijawahi kuonekana kokote na kuzusha taharuki ya kwa mashabiki na wadau mbalimbali lakini wakatoa ufafanuzi kwamba hizo sio jezi mpya kwa msimu ujao mzigo utakuja.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said ambao ndio wenye mamlaka katika kuzalisha na kuuza jezi za Yanga amesema jezi hizo zipo kwao muda mrefu ambazo ni maalum kwa ajili ya dharula katika mazoezi.

Hersi amesema jezi hizo ni maalum kwa ajili ya mazoezi pekee watakazotumia wakati wote wakiwa hapa ambapo pia wamekuja na zingine zitakazotumika nazo kwa ajili ya mazoezi.

Kigogo huyo amesema jezi maalum kwa msimu ujao ziko njiani ambazo zitakuwa kali kushinda zote ambazo wamewahi kuzileta nchini tangu wachukue zabuni ya kuzalisha jezi za Yanga.

Amesema jezi hizo hazitauzwa na kwamba watakaozitumia ni wachezaji pekee katika mazoezi yao na ndio maana hazina majina ya wachezaji wao.

"Hizi sio jezi za kuuzwa na wala sio jezi zetu mpya watu wasichanganye mambo kwa kuwa wameziona leo tunazitumia huku,"amesema Hersi ambaye naye alizivaa akifanya mazoezi pembeni.

"Jezi yetu mpya ya msimu ujao hatuwezi kuisambaza namna hii na hii jezi nikwambie ilikuja muda mrefu huko nyuma lakini tukasema tusiitumie sasa kuna wakati tulifikiria itumike katika mashindano ya Kagame lakini tukasema tutazitumia huku."