Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559954

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hoteli waliyofikia Yanga hii hapa

Hoteli waliyofikia Yanga hii hapa Hoteli waliyofikia Yanga hii hapa

KIKOSI cha Yanga kimefikia katika hoteli ya ELCT Bukoba hoteli iliyopo mjini itakaa hapo kwa hadi watakapo maliza mchezo na Kagera Sugar Jumatano.

Yanga wamepumzika hapo kwa muda na baadae watatoka kwaajili ya kwenda mazoezini ambapo kocha msaidizi Cedric Kaze amesema leo watafanya mazoezi mepesi ili kuweka mwili sawa.

Amesema wachezaji wamepumzika kwa muda lakini watakuwa na muda mchache wa kuweka miili sawa kwa kufanya mazoezi mepesi.

“Leo tutafanya mazoezi jioni na kesho tutafanya asubuhi lengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo wetu wa kwanza ugenini,” amesema na kuongeza kuwa;

“Wachezaji wapo kwenye hari nzuri ya mchezo tunatarajia matokeo mazuri kutoka kwao lengo likiwa ni kuhakikisha tunakusanya pointi zote tatu,” amesema.