Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553615

Soccer News of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Huu hapa uzi mpya wa Yanga 2021/2022

Viongozi wa Yanga wakizindua Jezi mpya za Yanga Viongozi wa Yanga wakizindua Jezi mpya za Yanga

Yanga leo Agost 24, katika Ukumbi wa Mlimani City wamezindua jezi aina kumi tofauti katika kuelekea msimu mpya 2021/2022.

Yanga wamezindua jezi za nyumbani na ugenini pamoja na third kit kama sheria inavyotaka, Lakini pia wamezindua jezi kwa ajili ya Mashindano ya Kimataifa nyumbani na ugenini ukizingatia Yanga itashiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Lakini vile vile Yanga imetambulisha jezi ambazo zitavaliwa na wachezaji wakati wa Mazoezi,watazovaa wachezaji wakati wa safari na zile za Transformation.

Akitaja bei za jezi hizo, Msemaji wa Mabingwa hao wa Kihistoria,Haji Manara amesema kwa bei ya Jumla ni shilingi 28000 na kwa reja reja popote pale nchini ni shilingi 35000.

Mbunifu wa Jezi hizo ni Mtanzania Sheria Ngowi, ambae alipata wasaa wa kuzielezea jezi hizo kwa Mahabiki, Wanachama na Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo.