Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 19Article 547465

Habari za michezo of Monday, 19 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Ihefu, Gwambina, JKT kwaheri …

Ihefu, Gwambina, JKT kwaheri  … Ihefu, Gwambina, JKT kwaheri …

TIMU za Ihefu, Gwambina, JKT Tanzania na Mwadui zimeaga Ligi Kuu Bara baada ya jana kushuka daraja katika mechi za mwisho.

Mwadui ilishashuka siku nyingi, ilikuwa ikisubiriwa kuona timu itakazoungana nazo ambazo zilijulikana jana baada ya msimu wa mwaka 2020/21 kumalizika.

Ihefu wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa KMC na kubaki katika nafasi ya 17 wakiwa na pointi 35, baada ya kushuka uwanjani mara 34.

Licha ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons na kufikisha pointi 35 baada ya michezo 34 hilo halijawasaidia Gwambina kuepuka mkono wa kwaheri hawatakuwa sehemu ya timu zitakazo shiriki Ligi Kuu Bara.

Upepo umebadilika kwa Coastal Union na Mtibwa Sugar ambazo zimesubiri hadi mchezo wa mwisho kuhakikisha kuwa zinapata nafasi ya kucheza mtoano dhidi ya walioshika nafasi za pili daraja la kwanza Pamba na Transit Camp.

Coastal ikiwa nyumbani Mkwakwani iliifunga Kagera Sugar mabao 3-1 na hivyo itacheza mtoano na Pamba keshokutwa na Mtibwa Sugar ilitoka sare ya bao 1-1 na JKT Tanzania na hivyo itacheza mtoano na Transit Camp mwishoni mwa wiki hii.

Sare ya JKT dhidi ya Mtibwa haikuwa na msaada kwani timu hiyo iliyo chini ya Abdallah Baresi imeshuka.