Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 20Article 573013

Soccer News of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ilulu hapatoshi, Namungo dhidi ya Yanga

Mashabiki wakisubiri mtanange baina ya Namungo na Yanga Mashabiki wakisubiri mtanange baina ya Namungo na Yanga

Ni balaa ndivyo unavyoweza kusema kwa jinsi mashabiki walivyojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ilulu kutazama mchezo kati ya Namungo na Yanga.

Yanga Iko ugenini mkoani Lindi kuikabili Namungo katika mchezo utakaoanza saa 10:00 jioni.

Hadi kufikia saa 6:00 mchana sehemu kubwa ya  Uwanja umejaa huku  nje bado kukiwa na idadi kubwa ya watu.

Mageti ya uwanjani yalifunguliwa kuanzia Saa 4:30 asubuhi na mashabiki kuanzia kuingia uwanjani lakini hadi kufikia saa sita mchana Uwanja  umefurika huku mashabiki wakiendelea kuingia.

Licha ya kwamba mechi inaanzia Saa 10 jioni lakini mashabiki hawajali kwamba watakaa muda mrefu kusubiri mchezo huo huku wale wa mzunguko wakipata tabu zaidi kwani jukwaa lao hakuna mahali pa kukaa Bali ni  mwendo wa kusimama hadi mpira unaisha.