Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 16Article 542902

Habari za michezo of Wednesday, 16 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ishu ya Bwalya kuja Simba imefikia hapa

Ishu ya Bwalya kuja Simba imefikia hapa Ishu ya Bwalya kuja Simba imefikia hapa

Ishu ya Bwalya kuja Simba imefikia hapa June 16, 2021 by Global PublishersSIMBA itapata ugumu wa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Al Ahly raia wa DR Congo, Walter Bwalya anayewaniwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Timu hiyo imepanga kukifanyia maboresho kikosi chao kwa kusajili beki wa kushoto, kati, kiungo na mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao.

Tayari timu hiyo imepeleka ofa ya kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo aliyekuwa anaichezea Nkana Rangers ya Zambia kabla ya kutua Al Ahly.

Kwa mujibu wa mmoja wa mtandao kutoka Afrika Kusini wakala wa Bwalya, anayefahamika kwa jina la Paricha Chikoye, amekiri kwamba ni kweli Al Ahly wanataka kumuuza mshambuliaji huyo Simba, lakini itakuwa ngumu kutokana na fedha.“Ni kweli Al Ahly wanataka kumuuza mteja wangu kutokana na kuona kwamba haendani na mfumo ya timu yao hivyo hamna namna lazima wamuuze.“

Awali ilikuwa tetesi kwamba anahitajika na Simba ila ukweli ni kwamba Simba hawana uwezo wa kumlipa fedha ambazo tunahitaji kutokana na mkataba wa kule Al Ahly.

“Kumpata Bwalya sio jambo jepesi na sisi tunahitaji fedha kubwa na siwezi kukutajia kwa sasa hivyo tusubiri na tuone,” alisema Chikoye.

STORI: WILBERT MOLANDI,Dar es Salaam