Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 03Article 540769

Soccer News of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Ishu ya Kahata Kusepa Simba ipo hivi

Ishu ya Kahata Kusepa Simba ipo hivi Ishu ya Kahata Kusepa Simba ipo hivi

Kiungo wa klabu ya Simba, Mkenya, Francis Kahata huenda akaondoka kwa wababe hao wa kariakoo baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku ikielezwa hatoongezewa mkataba na mabosi wake.

Submitted by George David on Alhamisi , 3rd Jun , 2021 Kiungo Francis Kahata akisakata kabumbu.

Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Kahata zimeeleza kwamba ujio wa Perfect Chikwende ni sababu ya kwanza kwa mabosi hao kuamua kumtomuongezea kandarasi mpya mkali huyo wa kupiga pasi za mbali kana kamba zimechotwa na kijiko.

Chanzo hicho kimesema "Kahata yupoyupo Simba ila hajaongeza mkataba kwa kuwa mabosi wamemgomea kwa sasa hivyo ataondoka Bongo muda wowote kuanzia sasa".

Alipotafutwa Kahata alisema kuwa anahitaji kupumzika kwanza kabla ya kuzungumza kuhusu suala hilo. Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo alishaanza kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuandamwa na majeraha ya mguu pamoja na ushindani mkubwa wa namba uliopo kikosini hapo hususani chini ya kocha wa Simba wa sasa mfaransa, Didier Gomez Da Rosa ambaye humtumia sana Larry Bwalya.

Ikumbukwe kuwa kiungo huyo alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya.

Join our Newsletter