Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 22Article 559024

Soccer News of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Israel Mwenda arithi mikoba ya Ame Simba SC

Beki wa Simba, Israel Mwenda Beki wa Simba, Israel Mwenda

Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba, Israel Mwenda amekabidhiwa jezi namba 5 iliyokuwa inavaliwa na beki chipukizi Ibrahim Ame.

Mwenda ameibukia ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes akitokea kikosi cha KMC.

Kwa sasa Ame yupo zake kwa mkopo ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar chenye ngome yake Morogoro akiendelea kupambana kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22.

Kikosi cha Simba, jana Septemba 21 kilirejea kambini baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili mara baada ya kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa.

Maandalizi ya wakati huu kwa Simba ni kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25, saa 11:00 jioni.