Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 08Article 556168

Soccer News of Wednesday, 8 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Itakua siku ya matukio Simba Day " - Kamwaga

Sehemu ya wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini Jjini Arusha Sehemu ya wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini Jjini Arusha

Kuelekea katika kilele cha tamasha la Simba Day, linalotarajiwa kufanyika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa, uongozi wa timu ya simba umesema maandalizi ya shughuli hiyo yamekamilika kwa asilimia zote.

Smba kwa sasa ipo Jijini Arusha ambako imeweka kambi ikijifua kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya 2021/2022 chini ya Kocha Didier Gomes.

Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa wanaendelea salama na mazoezi katika jiji la utalii Tanzania, Arusha.

"Kuelekea katika Simba Day kila kitu kipo sawa hivyo ni suala la mashabiki kuweza kujitokeza kwa wingi kuona namna itakavyokuwa siku hiyo na tunaamini watafurahi.

"Tayari jezi ipo sokoni na inapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei hivyo kila shabiki kwa sasa ni muda wake kuipata jezi hiyo ambayo ina ubora wa hali ya juu".

Septemba 13 inatarajiwa kuwa ni Wiki ya Simba ambapo watakuwa wakifanya matendo ya huruma kwa jamii pamoja na usafi, kwa kuwa jamii ni sehemu ya Simba SC.

Septemba 19 itakuwa ni siku ya tamasha rasmi ambapo mbali na kuwatambulisha wachezaji wao pia watatambulisha uzi na kutakuwa na mchezo kati ya Simba v TP Mazembe.