Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559978

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jamhuri Morogoro wafungiwa, wadau wadondoshea lawama Serikali

Jamhuri Morogoro wafungiwa, wadau wadondoshea lawama Serikali Jamhuri Morogoro wafungiwa, wadau wadondoshea lawama Serikali

Baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kukosa hadhi za kuchezea ligi kuu Tanzania bara msimu huu, wadau wa soka wameita kitendo hicho kuwa ni cha aibu.

Mdau wa soka nchini, Hashim Mbaga ameeleza kuwa ni kweli viongozi wa serikali mkoa, chama cha soka Morogoro na mwakilishi wa wananchi jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood wapo na wanaona jambo hilo likitokea, upande wake haamini kama viongozi hao wameshindwa kutatua ishu hiyo.

Mbaga alisema kuwa uwanja wa jamhuri umekosa hadhi ya kuchezewa mechi za ligi kuu mpaka michezo imehamishiwa kwenda uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.

Kwa maelezo hayo ya Mbaga, ujumbe huo umewalenga viongozi wakuu wa Chama cha Soka Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Wakili Albert Msando na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood ambao wanadaiwa kushindwa kuingilia jambo hilo kwa jicho la tatu ili kuepusha uwanja huo kufungiwa mara kwa mara.

Mbaga ambaye amewahi kuwa kuwa meneja wa klabu ya Simba na Mkurugenzi wa wanachama wa klabu hiyo. alisema mama alishasema kauli akimaanisha rais wa Tanzania, Rais Suluhu Hassa ametoa maelekezo viwanja vya michezo vifanyiwe marekebisho kwa ajili ya kutumika kwa michezo mbalimbali nchini hususani soka ambapo timu nyingi za ligi kuu Tanzania bara na madaraja mengine vinategemea kutumia viwanja vinavyomilikiwa na CCM.

Meneja wa uwanja huo, John Simkoko alisema wamekuwa wakifanya marekebisho ya mara kwa mara katika uwanja huo ambayo ni ya kawaida kwa viwanja vingine kufanyiwa marekebisho mara kwa mara.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheila Lukuba ametoa ushauri kwa mkuu wa wilaya ya Morogoro, Wakili Albert Msando kukaa na viongozi wa Chama tawala (CCM) ili kupata suluhu na kupata mwarobaini wa kukomesha tatizo linalopelekea uwanja huo uwe unafungiwa mara kwa mara.

Diwani wa kata ya Sultan Manispaa ya Morogoro, Samuel Msuya alisema ni aibu kwa uwanja wa jamhuri kufungiwa mara kwa mara.

“Ni aibu kubwa sana na viongozi wetu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro.”alisema Msuya. Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Martin Shigela na mkuu wa wilaya ya Morogoro, Wakili Albert Msando walipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi haikupokelewa juu ya viongozi hao kuingilia kati ukarabati wa uwanja huo.

Katibu wa chama cha soka mkoa wa Morogoro, Emmanuel Kimbawala alisema mchezo kati ya Mtibwa Sugar ambao walikuwa wenyeji dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Mbeya Kwanza umehamishiwa uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.