Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553063

Soccer News of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Jesus Moloko ni kitu kingine " - Injinia Hersi

Mchezaji mpya aliesajiliwa na Yanga Jesus Moloko Mchezaji mpya aliesajiliwa na Yanga Jesus Moloko

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said amesema winga mpya aliesajiliwa na Timu ya Yanga Jesus Moloko ni habari nyingine wanachotakiwa wanayanga ni wampe nafasi tu.

Hersi ameyasema hayo kufuatia mashaka ya mashabiki juu ya mchezaji huyo hasa ikionekana kama hana makeke mengi mazoezini.

"Nnachowaomba waniamini na niwahakikishie kuwa tumepata mtu, mtu kwa maana ya uwezo na niwahakikishie wamsubiri uwajani" amesema Hersi

"Wamelalamika kwa yule alieondoka (Tuisila), lakini wajue kuwa sisi tulimpata yule mchezaji kutoka kwa watu, sasa anapoonesha nia ya kuhitaji kwenda sehemu nyingine ilikua ni busara kumruhusu, tumetengeneza kiasi kikubwa cha pesa lakini hata hii kambi tuliyopo ni matunda ya biashara ya mauzo yake" amesisitiza Hersi

Winga Moloko ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliosajiliwa kuziba pengo la nyota aliyetimkia RS Berkane ya Morocco.