Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558364

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jezi Yanga zachangamkiwa Simba Day

Jezi Yanga zachangamkiwa Simba Day Jezi Yanga zachangamkiwa Simba Day

PALIPO na Simba, Yanga hawezi kukosekana hivyo ndio unaweza kusema baada ya wauzaji wa jezi kuibuka na kuweka wazi kuwa hawawezi kuuza jezi za timu hiyo pekee kwasababu hao ni mapacha.

Mwanahamis Richard ambaye ni muuzaji wa jezi nje ya uwanja wa Mkapa anasema leo ni siku maalum ya Simba lakini bado kuna mashabiki wa Yanga wanakuja kutoka mikoani wananunua.

“Kuna mwanaume au mwanamke anakuja na mtu wake na ni wapinzani hivyo mmoja ananunua ya Yanga na mwingine Simba biashara ipo na inafanyika vizuri,” anasema.

Pia kuna wazazi wanakuja na wanao wengine Simba na wengine Yanga tunauza pia hivyo ni ngumu sana ukaona tunabiashara ya upande mmoja tunajua namna changamoto hizi kwa watani.