Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 29Article 554194

Habari za michezo of Sunday, 29 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jezi mpya Yanga bei haikamatiki

Jezi mpya Yanga zalanguliwa Jezi mpya Yanga zalanguliwa

LICHA ya uongozi wa Yanga kutangaza bei rasmi ya kuuza jezi zao mpya ni Sh 35,000 lakini sasa uuzaji mtaani umepandishwa hadi Sh60,000 - 70,000 kwa moja.

Yanga walitangaza jezi mpya siku chache zilizopita lakini kutokana na mapokeo makubwa na Wanajangwani hao kununua jezi lakini imekuwa shida kutokana na jezi kuwa adimu.

Suleiman Hamad kutoka Morogoro amesema alitaka kupata jezi ya njano ambayo ina wananchi ndani yake lakini ameikosa,.

Amesema walitangaziwa jezi bei elekezi lakini kwa sasa jezi ya njano imekuwa lulu kwani hata makao makuu ya klabu hiyo kuna ya rangi nyeusi pekee.

"Mimi nimetoka Morogoro kuja hapa kupata jezi lakini imekuwa ngumu na shida kupata tunaambiwa imebakia nyeusi pekee Sh35,000 rangi nyingine hakuna, " amesema Hamad na kuongeza,

"Ila hao wanaouza hapo nje wanauza mpaka Sh70,000 ambayo sio bei sahihi kabisa sisi tunajitoa kuisapoti timu yetu lakini tunashangaa kinachofanyika," amesema.

Naye Omary Ally amesema "Hii sio sawa jezi zimekuwa adimu sanasana hasa hizi za njano maana ndio tumezipenda,"

Mmoja wa wauza jezi ambaye yupo nje ya makao makuu ya Yanga Salim Ngwale amesema sasa anauza Sh70,000 kwa kuwa ndiyo inayoonekana kupendwa zaidi. "Mimi mfanyabiashara natembelea nyota kwani wanaonekana wanaipenda sana na mimi napandisha, " "Mimi nimenunua Sh50,000 hivyo sina namna nauza Sh70,000 zile za njano hizo nyeusi nauza Sh60,000 zinaenda tu naomba GSM wawape kazi watu jezi ziwe nyingi," amesema Ngwale.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga, Injinia Hersi Said amesema, hata wao hawakutarajia kilichotokea katika mapokeo ya jezi hizo. Amesema walileta jezi za awali 60,000 ukiwa ni mzigo wa kwanza na mzigo mwingine huko njiani unakuja. "Sasa hivi jezi zimechukuliwa nyingi na wauzaji wa rejareja na ndio maana wanapandisha kwa bei hiyo lakini sisi bei yetu elekezi ndio hiyo Sh35,000," Aidha Hersi amesema kilichotokea jezi ya njano na kijani imeonekana kupendwa zaidi tofauti na makadilio yao. "Tunawaomba Wanayanga wawe watulivu mzigo unakuja na nchi nzima tumefika, tunawashukuru pia kwa namna ambayo wameichangamkia jezi yao pendwa tutaongeza nyingi kadri ya uwezo wetu," amesisitiza Hersi