Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584881

Mpira wa Kikapu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Joel Embiid aipaisha Philadephia Wakiichapa Rockets

Joel Embiid Joel Embiid

Ligi Kuu ya mpira wa kikapu NBA imeendelea usiku na alfajiri ya leo ikishuhudia michezo 7 katika viwanja tofauti tofauti.

Joel Embiid ameendelea kuuwasha moto akifunga points 31, rebounds 8 na aki assists mara 6 akiiwezesha Philadelphia 76ers kuichapa Houston Rockets kwa vikapu 111 dhidi ya 91.

Cade Cunningham alikua na wakati mzuri akifunga points 29 (points zake za juu kabisa), akiwa na mitupio 5 ya points 3, na kutoa assists mara 8 akiibeba Detroit Pistons kuifunga Uttah Jazz kwa points 126 dhidi ya 116.

Kwingineko Brooklyn Nets walikubali kipigo kutoka kwa Portland Trails Blazers cha points 114 kwa 108 huku alama moja tu ikiwabeba Cleveland Cavaliers dhidi ya Sacramento Kings 109 kwa 108.

Matokeo mengine ni kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini;