Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541372

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

John Bocco Agomea Kiatu cha Dhahabu

John Bocco Agomea Kiatu cha Dhahabu John Bocco Agomea Kiatu cha Dhahabu

John Bocco Agomea Kiatu cha Dhahabu June 7, 2021 by Global PublishersBAADA ya mshambuliaji wa Simba, John Bocco kufunga bao lake la 13 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu nahodha huyo wa Simba ameweka wazi kwamba kipaumbele chake ni kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa na siyo kupambana kuchukua kiatu cha ufungaji bora.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wenzangu kwa kupambana na kupata matokeo mbele ya Ruvu Shooting, ulikua mchezo mgumu ambao tulitakiwa kushinda na tutaendelea kupambana mpaka tone la mwisho kwani malengo ni kunyakua ubingwa wa ligi kuu.“Kutwaa kiatu cha ufungaji bora katika ligi kuu kwangu siyo kipaumbele badala yake malengo yangu ni kuhakikisha kwamba napigana ili Simba itwae ubingwa na kama ikitokea nimefunga mabao mengi basi nitachukua hizo zawadi lakini kwa sasa malengo yangu ni kuisaidia Simba kutwaa ubingwa na sio vingine vinginevyo.”

Stori: Johnson James | Championi

Join our Newsletter