Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 26Article 559711

Boxing News of Sunday, 26 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Joshua apigwa na kupoteza mikanda yote

Joshua apigwa na kupoteza mikanda yote Joshua apigwa na kupoteza mikanda yote

Bondia Oleksander Usyk wa Ukraine amemdunda Anthony Joshua wa England kwenye pambano lililofanyika kwenye dimba la Tottenham Hotspurs usiku wa kuamkia leo Septemba 26, 2021.

Ushindi huo umemfanya Usyk abebe mikanda yote ya uzito wa juu wa Super WBA, WBO na IBF aliyokuwa anaishikilia Joshua.

Pambano la 19 kwa Usyk, 13 akishinda kwa KO akiwa hajawahi kupigwa hata pambano moja.

Usyk akitangazwa mshindi

Joshua alipanga amtafute Tyson Fury ili wazichape kugombania mkanda wa WBC ambao ni wa uzito wa juu lakini mambo yamebadilika sasa hana mkanda hata mmoja.

Ikumbukwe kuwa Anthony Joshua ndiye mwanadamu pekee aliyewahi beba mikanda minne ya Uzito wa Cruise Weight ndani ya mapambano 15 tu.

Usyk zkiwa na mikanda yake

Akapanda uzito kwenda Heavy Weight na mapambano manne tu akawa kinara na bingwa wa uzani wa juu akishikilia mikanda mitatu WBA , IBF na WBO.

Rekodi za Oleksander Usyk mwenye miaka 34 Mapambano 19  Ushindi 19 KO 13