Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 560002

Boxing News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Joshua na Mtihani mzito Kurudisha Mikanda yake

Antony Joshua (kulia) akiwa na Oleksandr Usyk mara baada ya Pambano lao Antony Joshua (kulia) akiwa na Oleksandr Usyk mara baada ya Pambano lao

Anthony Joshua ana kazi kubwa ya kujijenga upya kukabili kisasi dhidi ya bondia wa kipaji cha dunia nyingine Oleksandr Usyk - anaweza kurudi upya tena ?

Antony Joshua ana maswali ya kujiuliza kufuatia kupoteza pambano la pili ambalo hata hivyo halifanani na pambano lake la kwanza alilopoteza.

Mara ya mwisho kupoteza alikua maelfu ya maili, mbali na nyumbani alikua mgeni katika ardhi ya ugenini. Alikumbana na makonde mfululizo ambayo alijua na aliamini haitotokea ijirudie tena.

Alipata wasaa wa kupotelea New York kwa siku kadhaa baada ya kamera na kelele za Mashabiki kuondoka, kutafakari kuhusu uliokuwa usiku wake mbaya zaidi, na kujiuliza alikosea wapi.

Wakati huu mambo ni tofauti. Tofauti kabisa. Kivuli cha Uwanja wa Tottenham Hotspurs kinaangaza majengo ya Halmshauri alikotokea, Gym yake ya kwanza kwenda wakati akifanya mazoezi, Klabu za usiku alizokuwa anakwenda wakati akiwa kijana mdogo.

Sasa hivi mahali pa kutafakari upya namna atakavyorudisha ubingwa wake wa dunia kwa mara ya pili ni nyuma ya Nyumba yake.

Fikra ambazo zitatawaliwa na picha ya mgeni, mgeni ambae tabasamu lake huenda likazidi kuziwinda ndoto za Antony Joshua kwa muda mrefu sana.

Oleksandr Usyk kwa utulivu kabisa usiku wa Jumamosi alijaribu kumkumbusha Joshua kuwa mipango yake mikubwa haikuwa sahihi kufikiria ushindi kama ilivyokuwa kwa Andy Ruiz Jr mwaka 2019.

Usyk ni uzao tofauti kabisa, na bado tuko katika mchakato wa kujifunza maverick huyu mwenye busara na masharubu ni nani hasa.

Mbele yake sasa Joshua ana mtu ambaye alimshinda kikamilifu na ambaye hata alidai kwamba mkufunzi wake alimshauri asimpige bingwa.