Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 30Article 560554

Soccer News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Juve yaishangaza Chelesa

Winga wa Juve, Federico Chiessa akimtoka beki wa Chelsea Winga wa Juve, Federico Chiessa akimtoka beki wa Chelsea

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, klabu ya Chelsea usiku wa jana wamekumbana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa vibibi vizee vya Turin, klabu ya Juvetus.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Allianz nchini Italia, lilishuhudia mabingwa hao wa msimu uliopita wakiondoka wanyonge kutoka kwa vijana wa Masimiliano Allegri.

Goli pekee la Juventus katika mchezo huo limefungwa na F. Chiesa 46, na kuwafanya Chelsea kupoteza Pointi tatu.

Katika mchezo mwingine wa Kundi H, Klabu ya Zenit imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Malmo FF.