Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 23Article 559153

Soccer News of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Juventus yashinda mechi ya kwanza Serie A

Wachezaji wa Juventus wakimpongeza Mathias de Light baada ya kufunga bao la ushindi Wachezaji wa Juventus wakimpongeza Mathias de Light baada ya kufunga bao la ushindi

Kibibi kizee cha Turin, Klabu ya Juventus wamepata ushindi wao wa kwanza ndani ya Serie A tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2021/2022 dhidi ya Spezia.

Juventus ambao waliukosa ubingwa wa Serie A msimu uliopita baada ya kuubeba mara tisa mfululizo, hawakushinda mechi yoyote msimu huu ndani ya mechi nne za mwanzo wa Ligi walizocheza ambapo walitoa sare mechi mbili na kupoteza mechi mbili.

Magoli ya Juventus usiku wa jana yamefungwa na kinda Moise Kean 28', F. Chiesa 66' na beki M. de Light 72'.

Magoli ya Spezia yamewekwa kimiani na E. Q. Gyas dakika ya 33 na J. Antiste dakika ya 49 ya mchezo.

Mpaka dakika 90 zinakamilika, Juve wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 angalau kutoa ahueni kwa kocha wa timu hiyo Masimiliano Allegri.