Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 20Article 572986

Soccer News of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

KDB akutwa na Covid

KDB akutwa na Covid KDB akutwa na Covid

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona na anatarajiwa kukosa mechi za timu yake ya Manchester City takribani tatu zijazo.

Kiungo huyo alikutwa na maambukizi hayo juzi Jumatano baada ya kufanyiwa vipimo wakati akirejea katika majukumu ya klabu akitokea timu ya taifa ya Ubelgiji, ambapo sasa atalazimika kujitenga kwa siku kumi.

Hiyo inamaanisha kuwa kocha wa City, Pep Guardiola atamkosa staa huyo katika mchezo dhidi ya Everton kwenye Premier League kisha dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye UEFA Champions League.