Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573298

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KMC yaandika historia msimu huu

Azam wanyonge mbele ya KMC Azam wanyonge mbele ya KMC

Baada ya kucheza mechi tano bila ushindi hatimaye bao la dakika ya 90 lililofungwa na Hassan Kabunda limetosha kuipa ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu KMC FC kkiichapa Azam 2-1 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kucheza kwa tahadhari huku wenyeji KMC wakionekana kumiliki mpira kuliko wapinzani wao, Azam.

Dakika 12 zilitosha kwa KMC kuandika bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wake, Matheo Antony kwa Kiki kali iliyomshinda kudaka kipa wa Azam Mathias Kigonya na kuzama nyavuni.

Bao hilo lilikuwa kama chachu kwa KMC kwani wachezaji wake waliendelea kucheza kwa kutulia huku wakilisakama lango la Azam lakini hadi kufika dakika ya 30 matokeo yalikuwa bado hayajabadilika.

Azam nao walitengeneza baadhi ya nafasi za kufunga lakini jitihada zao zilikwamia kwenye ukuta wa KMC chini ya nahodha Sadala Lipangile hadi kufika dakika ya 40.

Dakika ya 43, Azam walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Charles Zulu aliyepiga Kiki kali nje ya boksi la 18 la KMC na mpira kuzama moja kwa moja nyavuni na kupindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili kilirejea kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo kwa Azam waliingia Keneth Muguna na Rogers Kola kuchukua nafasi za Idris Mbombo na Never Tigere huku Mohammed Samatta, Martin Kigi, na Hassan Kabunda wakiingia kwa Kmc kuchukua nafasi za Emmanuel Mvuyekure, Miraji Athuman, na Abdul Hilaly.

Mabadiliko hayo yalifanya mchezo kubadilika kwa pande zote mbili kushambuliana kwa kupokezana lakini hadi kufika dakika ya 80 matokeo yalibaki kuwa 1-1.

Dakika ya 90, KMC walipata bao la pili kupitia kwa Hassan Kabunda ambalo liliipa ushindi timu hiyo iliyokuwa nyumbani katika mchezo huo na kufikisha point tano ikipanda hadi nafasi ya 15 kutoka ya mwisho (16) iliyokuwepo awali.