Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573142

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kaburu ajitokeza mkutano mkuu Simba

Kaburu ajitokeza mkutano mkuu Simba Kaburu ajitokeza mkutano mkuu Simba

Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geodfrey Nyange 'Kaburu' ni miongoni mwa wanachama waliojitokeza kwenye mkutano mkuu wa Simba unaoendelea katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Kaburu amewasili kwenye mkutano huo saa 4:02 asubuhi na kwenda kukaa kwenye moja ya viti vya mbele vya ukumbi wa Mwalimu Nyerere unapofanyika mkutano huo.

Baada ya kuketi, baadhi ya wanachama walikwenda kumsabahi na wengine kuibua minong'ono.