Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552655

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kabwili, Mauya wachekelea kuitwa Stars

Ramadhan Kabwili Ramadhan Kabwili

Kiungo Zawadi Mauya na kipa Ramadhan Kabwili wameonyesha kufurahia hatua ya kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars lakini wakajipanga kuhakikisha wanadumu katika timu hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mauya ambaye ni mara ya kwanza anaitwa Stars amesema amepata faraja ya kuona sasa anapata nafasi ya kulitumikia Taifa na kwamba kwenda kwake katika timu hiyo anataka kuhakikisha anajituma ili acheze katika mechi hizo mbili za kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.

"Nimefarijika sana unajua sikuwahi kuitwa timu hii ya Taifa Stars naishukuru Yanga kwa kunipa nafasi ya kuonekana hii hainifanyi kuridhika nitakwenda kupambana ili sasa nicheze na niendelee kubaki kuitwa kila wakati,"amesema Mauya.

Naye kipa Ramadhan Kabwili amesema kurudi kwake kufanya kazi chini ya kocha wa Stars Kim Poulsen kimempa nguvu ya kuhakikisha kwamba sasa anatakiwa kuanza msimu kwa kucheza ndani ya klabu yake.

"Sijacheza muda mrefu lakini bado najijua nina ubora na kocha ananiamini hii inanifanya sasa kwenda kupambana zaidi kule Stars lakini pia hata huku Yanga msimu ndio unaanza nataka kuhakikisha najituma ili nianze kupata mechi za kucheza,"amesema Kabwili.

Stars inaingia kambini Agosti 24 kujiandaa na michezo miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Madagascar na DR.Congo.