Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 19Article 558301

Habari za michezo of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kader aitanguliza Azam FC

Kader aitanguliza Azam FC Kader aitanguliza Azam FC

BAO la kiungo mshambuliaji Ismail Aziz 'Kader' dakika ya 38, limeipa utangulizi timu ya Azam dhidi ya Horseed SC kutoka Somalia.

Mchezo huo unaopigwa katika Uwanja wa Azam Complex ulianza taratibu huku kila timu ikicheza kwa tahadhari na kushambulia kwa kushitukiza.

Azam ambayo ndiyo wageni katika mchezo huo wameonekana kutengeneza nafasi za wazi zaidi kuliko wenyeji wao Horssed ambao wameonekana kukosa muunganiko mzuri hasa wanapopeleka mashambulizi mbele.

Kada ambaye ndiye mfungaji pekee mpaka sasa ameonekana kuwa hatari katika ngome ya Horseed pamoja na Idd Nado wakitokea upande wa kulia na kushoto.

Horseed wana kazi ya kufanya katika kipindi cha pili kwani wana mlima wa kupanda kutokana na matokeo ya awali kupoteza kwa mabao 3-1, hivyo kufanya mchezo kuwa jumla ya mabao 4-1.

Nahodha wa Azam FC Salum Abubakar 'Sure Boy' ameonekana kutawala eneo la kiungo na kuwanyima nafasi wapinzani wao kupenya kwa golikipa Mathias Kigonya.